• Malalamiko |
    • MAWASILIANO |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Wafanyakazi |
Kaliua District Council
Kaliua District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu, na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Usafi wa Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Legal Unity
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji

Elimu Msingi



IDARA YA ELIMU MSINGI


Elimu ya Awali

          Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina madarasa 100 ya elimu ya awali na yote yanamilikiwa na serikali ya Tanzania. Madarasa haya ya elimu ya awali yana jumla ya wanafunanzi 12,172. Jedwali Na 1 hapa chini linaonesha mgawanyiko wa wanafunzi hao kwa jinsi 

Jedwali Na 1: Idadi ya Wanafunzi wa Elimu ya Awali kwa jinsi

Na
Idadi ya madarasa
Wav
Was
Jumla
1
100
6,076
6,096
12,172


Jedwali Na 2 hapa chini linaonesha kuwa kuna walimu 113 kwa ajili ya madarasa ya elimu ya awali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Jedwali Na 2: Idadi ya Walimu wa Elimu ya Awali kwa jinsi

Na
Idadi ya madarasa
Wanaume
Wanawake
Jumla
1
100
50
63
113


Elimu ya Msingi

Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina shule za msingi 100 na zote zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania. Idadi ya wanafunzi wote wa shule za msingi ni 76,502. Jedwali Na 3 hapa chini linaonesha idadi ya shule na wanafunzi kwa jinsi.

Jedwali Na 3: Idadi ya Shule na Wanafunzi kwa jinsi

Na
Idadi ya Shule
Wav
Was
Jumla
1
100
39,162
37,340
76,502


Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina walimu wa shule za msingi 1,663 kama Jedwali Na 4 hapa chini linavyoonesha.

Jedwali Na 4: Idadi ya Walimu wa Shule za Msingi kwa jinsi

  • Na
  • Idadi ya Shule
  • Wanaume
  • Wanawake
  • Jumla
  • 1
  • 100
  • 1,087
  • 576
  • 1,663


  • Mahitaji ya miundombinu na samani katika shule za msingi yameoneshwa katika Jedwali Na 5 hapa
  • Na
  • Aina
  • Mahitaji
  • Iliyopo
  • Upungufu
  • % upungufu
  • 1
  • Madarasa
  •   2,139
  •      681
  • 1,458
  • 68.2
  • 2
  • Nyumba za Walimu
  •   1,773
  •      326
  • 1,447
  • 81.6
  • 3
  • Matundu ya Vyoo
  •   4,128
  •      923
  • 3,205
  • 77.6
  • 4
  • Madawati
  • 29,664
  • 21,535
  • 8,129
  • 27.4

                           Jedwali Na 5: Mahitaji ya Miundombinu na Samani Shuleni


  • Ufaulu katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) na Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) unaoneshwa katika Jedwali Na 6 hapa chini kwa asilimia.
  • Jedwali Na 6: Ufaulu katika Mitihani ya Kitaifa kwa Asilimia
    • Na
    • Aina ya Mtihani
    • Ufaulu
    • 2013
    • 2014
    • 2015
    • 2016
    • 1
    • PSLE
    • 41.4
    • 41.0
    • 57.1
    • 82.3
    • 2
    • SFNA
    • 78.6
    • 80.9
    • 91.2
    • 98.0

    •  
    • Elimu Maalum
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina wanafunzi 275 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kama wanavyoainishwa katika Jedwali Na 7 hapa chini.
    • Na
    • Aina ya Ulemavu
    • Boys
    • Girls
    • Total
    • 1
    • Albino
    •     2
    •   3
    •     5
    • 2
    • Viziwi
    •   16
    • 13
    •   29
    • 3
    • Uoni Hafifu
    •   24
    • 15
    •   39
    • 4
    • Ulemavu wa Viungo
    •   98
    • 46
    • 144
    • 5
    • Ulemavu wa Akili
    •   29
    • 16
    •   45
    • 6
    • Usonji
    •   11
    •   2
    •   13

    • Jumla
    • 180
    • 95
    • 275

    Jedwali Na 7: Idadi ya Wanafunzi wenye Ulemavu


    • Kuna vitengo viwili kwa ajili wanafunzi wenye ulemavu ambavyo ni Shule ya Msingi Kaliua na Shule ya Msingi Milambo. Kitengo cha Shule ya Msingi Kaliua kinashughulika na wanafunzi wenye ulemavu wa ukiziwi. Kitengo hiki kina wanafunzi 7 wakiwemo wavulana 4 na wasichana 3. Kitengo cha Shule ya Msingi Milambo kinashughulika na wanafunzi wenye ulemavu wa akili. Kitengo hiki kina wanafunzi 11 wakiwemo wavulana 8 na wasichana 3.
    • Idadi ya walimu wenye taaluma ya elimu maalum katika Halmashauri ni 12 ambapo wanaume 9 na wanawake 3. Aidha, kuna walimu 11 wenye ulemavu ambapo wanaume ni 9 na wanawake 2.
    • Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua vilevile hushughulikia elimu nje ya mfumo rasmi. Kuna vituo 13 vyenye madarasa ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA). Vituo hivi hushughulika na watoto waliopo katika jamii ambao hawapo shuleni ili waweze kupata elimu ya msingi nje ya mfumo rasmi.
    • Idadi ya wanafunzi wa MEMKWA ni 596 wakiwemo wavulana 368 na wasichana 228. Walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA ni 13 wakiwemo wanawake 4 na wanaume 9.
    • Utekelezaji wa Miradi kwa Mwaka 2016/2017
    • Miradi inayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na ukarabati.
    • Madarasa 19 na matundu 18 ya vyoo yanajengwa kwa fedha ya Lipa Kulingana na Matokeo (P4R). Madarasa 12 yanakamilishwa kwa fedha ya ruzuku ya maendeleo (CDG) na madarasa 24 yanaezekwa kwa mabati yaliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Ukarabati wa darasa unafanyika shule ya msingi Pozamoyo kwa fedha ya P4R.

    • Shughuli ya kuezeka darasa kwa fedha za CDG zinaendelea shule ya Msingi Mkilig

    • Madarasa yaliyokamilishwa kwa fedha CDG Shule ya Msingi Busondi
    •  
  • Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T)


    • Mpango huu unafadhiliwa na nchi ya Uingereza kupitia Shirika la Kimataifa liitwalo UKAID. Lengo la mpango huu ni kuinua ubora wa elimu ya msingi Tanzania katika mikoa saba ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Mara, Shinyanga, Simiyu na Tabora.
    • Kutokana na kutekelezwa kwa mpango huu, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imenufaika ifuatavyo:
    • Maafisa Elimu Kata wamekuwa na uwezo kuzifikia shule ndani ya kata zao mara kwa mara kutokana na kupatiwa usafiri wa pikipiki na mafuta kila mwezi
    • Walimu wapatao 1700 wamejengewa uwezo wa kutumia mbinu bora za ufundishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili na kuwezesha wanafunzi wengi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu
    • Uanzishwaji wa vituo vya utayari wa kuanza shule umesaidia watoto wengi kuanza darasa la kwanza kwa umri unaotakiwa
    • Ushiriki wa jamii shughuli mbalimbali za shule umeongezeka kutokana kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWW) shuleni

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KALIUA DC MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II November 17, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • Ona zote

Habari za Hivipunde

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA WA MTAMBO DARAJA LA II {GREDA} NAFASI 01

    May 04, 2025
  • MNADA WA KWANZA WA ZAO LA KARANGA WILAYA YA KALIUA

    March 24, 2025
  • MADIWANI KALIUA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA BAJETI YA BILION 50.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    January 30, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUPITIA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII IMETOA HUNDI YA TSH. 302,000,000/=

    December 23, 2024
  • Ona zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Kaliua 2018
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mwanzo
  • TAMISEMI
  • Huduma
  • Historia
  • Fursa za Uwekezaji
  • UTUMISHI

Kurasa zinazofanana

  • Salary Slips Portal
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya RC Tabora
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti za Serikali
  • Baraza la Mitihani - NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

MAWASILIANO

    Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni

    Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua

    Simu: +255262965676/9

    Dawati la Uwekezaji:

    Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz

Dawati la Malamiko

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Service

Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua