Dira: Dira ya Sekta ya afya ni kuinua afya na ustawi wa wananchi hasa wale walioko kwenye hatari zaidi ya kuathirika na magonjwa kwa kukuza na kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi.
Dhamira/Taswira: Matarajio ni kutoa huduma muhimu za afya kwa gharama nafuu na zenye ubora na uwiano unaokubalika,zinazozingatia jinsia,endelevu na zinazolenga kuinua hali ya afya ya wananchi wa Wilaya ya Kaliua
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina vituo vya Afya vipatavyo 3 na jumla ya Zahanati 33 kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini. Kwa sasa halmashauri ya wilaya ya Kaliua inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayotarajiwa kuhudumia idadi ya watu wanaokadiriwa kufika 474,497 kwa makadirio ya mwaka 2016 Ongezeko la idadi ya watu ni 4% na kaya zilizopo ni 75,460 Kati ya hao watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ni 94,899 na kina mama walio kati ya umri wa miaka 15 – 49 ni 85,409.
MMILIKI |
HOSPITALI |
VITUO VYA AFYA |
ZAHANATI |
Vituo Vya Serikali
|
O |
3 |
33 |
Vituo Binafsi
|
O |
0 |
1 |
Vituo Vya Taasis ya Dini
|
0 |
1 |
2 |
Jumla
|
0 |
4 |
36 |
Kwa sasa kiwango cha uchanjaji ni 95% na kiwango cha utapiamlo kwa watoto ni 4%. Kiwango cha vifo vya akina mama ni 153/100,00. Kiwango cha akina mama wanaotumia uzazi wa mpango ni 24%. Kiwango cha maambukizi ya malaria ni 56%.
Watumishi
Idara ya afya hadi sasa ina jumla ya watumishi 146 wa kada mbalimbali (wauuguzi 55, wahudumu wa Afya 43, Maafisa wauguzi wasaidizi 16,Wauguzi 52, Matabibu 14, Makatibu wa Afya 2, watekinolojia maabara 9, maafisa afya mazingira 5, daktari msaidizi 1, afisa ustawi 1 na Daktari 3) ambayo ni sawa na asilimia 25 kati ya watumishi 580 wanaohitajika hivyo tuna upungufu wa watumishi 434 ambayo ni sawa na asilimia 75.
Huduma zinazotolewa kupitia vituo vya kutolea huduma
Na.
|
Huduma tolewa
|
Idadi ya vituo
|
1
|
Huduma za wagonjwa wa nje
|
36
|
2
|
Huduma za wangonjwa wa ndani
|
4
|
3
|
Huduma za Afya ya Uzazi Mama na Mtoto
|
36
|
4
|
Huduma za CTC
|
9
|
5
|
Huduma za PMTCT
|
38
|
6
|
Huduma za Chanjo
|
37
|
7
|
Huduma za upasuaji
|
1
|
8
|
Huduma za damu salama
|
1
|
WADAU WA MAENDELEO NA KAZI WANAZOFANYA
Idara ina wadau mbalimbali wanaosapoti huduma mbalimbambali zitolewazo katika idara ya Afya wadau hao ni kama ifuatavyo katika jedwali:-
S/N |
JINA LA MDAU WA MAENDELEO |
JINA LA MRADI |
KAZI WANAZOFANYA |
|
|
||||
1 |
Health Sector Basket Fund |
Health Sector Basket Fund
|
Kuboresha Huduma za Afya
|
|
2 |
World Bank |
Uimarishaji wa Afya ya Msingi kwa kuzingatia matokeo
|
Kuboresha miundo mbinu ya vituo na kutoa malipo kwa ufanisi wa utendaji kazi katika kutoa huduma za Afya
|
|
3 |
EGPAF |
Afya boresha maisha
|
Kuzuia Maambukuzi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, TB, Huduma za Uzazi wa Mpango, Kutoa elimu ya Afya na kusapoti vifaa tiba
|
|
4 |
IMA WORLD HEALTH |
Neglected Tropical Deseases Control Programme
|
Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele
|
|
5 |
JIPHIEGO-SAUTI |
Tohara ya kitabibu ya hiari kwa wanaume
|
Kufanya Tohara kwa wanaume
|
|
6 |
Global Fund |
kusapoti shughuli za Kifua Kikuu na UKIMWI
|
Kupunguza Maambukizi ya Kifua Kikuu na UKIMWI
|
|
7 |
EGENDER HEALTH |
Afya ya uzazi mama na mtoto
|
Kusapoti huduma za uzazi wa mpango wilayani
|
|
8 |
UNHCR (TCRS) |
Kuboresha duduma ya Afya ya Msingi
|
Kusapoti vituo vya Tarafa ya Ulyankulu makazi na ukarabati wa nyumba za watumishi na gari la wagonjwa
|
|
9 |
Mkapa Foundation |
Kujengea uwezo viongozi sekta ya Afya
|
Kujengea uwezo watumishi
|
|
10 |
Marie stopes |
Afya ya uzazi mama na mtoto
|
Kusapoti huduma za uzazi wa mpango wilayani
|
|
11 |
PIS |
Kuthibiti/Kupunguza Maambukizi ya VVU katika Jamii
|
Kusapoti dhana za kujikinga na mambukizi ya VVU
|
|
|
|
|
|
|
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua