Wilaya ya Kaliua ni kati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nane za Tabora na ilianzishwa Machi 2, 2012 na kuanza kazi yake kamili tarehe 14 Agosti 2013. Kabla ya kuanzishwa Kaliua na Ulyankulu zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Urambo. Eneo hilo lilikua kubwa kuwa chini ya Wilaya hiyo (Urambo) na kusababisha mapungifu katika utoaji wa huduma bora za jamii.
Kutokana na Ujumbe wa dira na dhima ya sasa, yafuatazo ni malengo makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua: -
A. Kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya VVU / UKIMWI
B. Kuimarisha, kutekeleza kwa ufanisi mkakati wa Taifa wa Kupambana na rushwa
C. Kuboresha upatikanaji wa huduma bora na usawa wa huduma za jamii
D. Kuongeza ubora wa huduma za kijamii na miundombinu
E. Kuongeza utawala bora na huduma za Utawala
F. Kuboresha ustawi wa jamii, Jinsia na Uwezeshaji
G. Umeimarishaji wa usimamizi wa maafa na dharura
Makao makuu ya Wilaya ya Kaliua yako katika mji wa Kaliua, kilomita 125 kutoka Manispaa ya Tabora.Wilaya hii inapakana na Urambo na Wilaya ya Uyui katika sehemu ya mashariki, Wilaya ya Mpanda na Mlele (mkoa wa Katavi) katika upande wa Kusini, Uvinza na Kibondo (Mkoa wa Kigoma) Magharibi. Upande wa Kaskazini wa Wilaya umepakana na Ushetu (Mkoa wa Shinyanga) na Bukombe (mkoa wa Geita) kaskazini magharibi.
Wilaya ya Kaliua ina eneo la ardhi la jumla ya kilomita za mraba 14,050 ambayo ni karibu 18.82% ya eneo la jumla la Tabora. Sehemu ya kilimo ni 1,965.5 kilimita za mraba kati ya hizo ni 1,500 kilomita za mraba hulimwa kila mwaka. Zilizo baki 12,084.5 (86%) ni hifadhi ya misitu, maeneo ya kawaida ya majani na maji. Uoto wa wilaya umegawanyika katika misitu ya asili ya miombo inayopatikana Igombenkulu, Milambo na Kanindo.
Joto ridi ni nyuzi joto za sentigredi 16-33 na msimu wa kiangazi ni mwezi wa Agosti na Oktoba. Wilaya inapata mvua kati ya 900-1300mm kila mwaka.
Viwango vya ukuaji idadi ya watu kwa kila mwaka kwa wilaya ya Kaliua ni takribani 4.8%. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, wilaya ilikuwa na watu 393,358 ambao wanawake wapatao 196,989 (50.1%) na wanaume 196,369 (49.9%). Kwa mwaka 2015 Wilaya inakadiriwa kuwa na watu 452,764 ambao 226,025 wanaume na 226,739 ni wanawake
Chanzo kikubwa cha mapato katika wilaya ya Kaliua ni biashara ya mazao ya kila mwaka ya mahindi (mahindi, maharagwe, mhoji na viazi vitamu) na mazao ya biashara (tumbaku, karanga, pamba, alizeti), bidhaa za msitu, asali na mifugo. Sekta ya kilimo huajiri asilimia 80 ya idadi ya watu wa Kaliua. Huduma za kijamii na kiuchumi zinatolewa na Serikali kwa ushirirkiano wa pamoja na sekta binafsi. Mapato kutoka kwa mifugo, uvuvi, asali, viwanda vidogo vya madini yanachangia mapato ya kaya
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imeanzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Namba 7 ya 1982, sehemu ya 8 na 9 na kurekebishwa na Sheria ya 6 ya 1999.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua