Wilaya ya Kaliua ina jumla ya Shule za Msingi 137 zenye vyumba vya madarasa 1268. Idadi hii inafanya uwiano wa chumba kwa wanafunzi kuwa 1:126 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa wa 1:45. Jumla ya vyumba vinavyohitajika ni 1,730 hivyo kufanya kuwa na upungufu wa vyumba 2277.
Madawati ya wanafunzi yaliyopo ni 43020 na hivyo kufanya uwiano wa dawati kwa wanafunzi kuwa 1:4 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa ambao ni 1:3. Idadi ya walimu waliopo ni 1771 kati yao wanawake ni 623 na wanaume ni 1,149. Idadi hii inafanya uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kuwa 1:90. Aidha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni 1:4.
Kwa upande wa nyumba za walimu, kuna nyumba 373 wakati mahitaji ni nyumba 1,771. Aidha matundu ya vyoo kwa wanafunzi yapo 1668 ukilinganisha na mahitaji ya matundu 6876.
Kwa wastani udahili wa wanafunzi kiwilaya upo katika kiwango cha 108% wakati kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la VII ni 82% na darasa la IV ni 84%
Kwa upande wa elimu ya watu wazima, kuna wanafunzi 578 waliojiunga na madarasa ya MEMKWA. Aidha Wilaya ina Chuo kimoja (1) cha ufundi stadi (VETA) ambacho kipo eneo la Ulyankulu.
Kiwango cha watu wanaojua kusoma na kuandika katika umri wa miaka 5 na kuendelea ni 82%.
Jitihada zaidi zinahitajika ili kuboresha huduma za Elimu katika Wilaya ya Kaliua.
Wilaya ya Kaliua ina jumla ya Shule za Sekondari 31 zenye vyumba vya madarasa 503. Idadi hii ya vyumba vya madarasa inafanya uwiano wa darasa kwa wanafunzi kuwa 1:41 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa ambao ni 1:40 hivyo kufanya wilaya kuwa na upungufu wa madarasa 13. Japo baadhi ya Shule zenye wanafunzi wengi zina uwiano mkubwa zaidi.
Kati ya kata zote 28 za kielimu zina shule za Sekondari kwa kuzingatia sera ya Elimu kila kata kuwa na shule ya sekondari, pia baadhi ya kata kulingana na wingi wa wanafunzi na ukubwa wa kata sasa kumekuwa na shule 2 ambazo ni Igwisi na Kaliua. Kata ya Igagala kuna Shule ya wasichana ya Mkoa (Dr. Batilda Burian) . Aidha ujenzi wa shule za sekondari mpya katika Kata 5 unaendelea ambapo kata hizo ni Milambo, Usinge, Ushokola, Igagala na Igwisi. Maabara zilizopo kwa sasa ni 87 ambapo kwa shule zilizopo zinatosheleza mahitaji. Kwa upande wa nyumba za walimu kuna jumla ya nyumba 98 wakati mahitaji halisi ni 429. .
Idadi ya walimu wa sekondari waliopo ni 429 na kati yao walimu 347 ni wanaume na 82 ni wanawake. Idadi hii ya walimu inafanya uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kuwa 1:16. Uwiano wa kitabu kwa wanafunzi ni 1:2 kwa vitabu vya masomo ya sayansi na 1:4 kwa masomo ya sanaa. Idadi ya viti vya wanafunzi vilivyopo ni 15464 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 497.
Kwa upande wa mabweni, Wilaya ina jumla ya mabweni 20 kati ya mahitaji ya mabweni 32. Aidha kiwango cha wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito ni 0.04%. Kwa wastani ufaulu wa mitihani ya taifa kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni 94%, kidato cha sita ni 100% wakati ufaulu kwa kidato cha pili uko katika kiwango cha 87%.
Jitihada zaidi zinahitajika ili kuboresha ubora wa elimu ya Sekondari katika Wilaya ya Kaliua.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua