KITENGO CHA SHERIA
Kitengo cha sharia kina majukumu ya kusimamia kesi zote ambazo aidha halmashauri imeshitaki au imeshitakiwa Mahakamani. Katika kutekeleza majukumu hayo kitengo cha sheria pia kitatoa ushauri kwa Halmashauri juu ya nini kifanyanyike ili kutoiletea hasara Halmashauri ambapo inasisitizwa kesi ambazo zinaweza kutatuliwa nje ya Mahakama zitatuliwe ili kuokoa muda lakini pia kupunguza gharama za kuendesha kesi.
Kazi zingine za kitengo ni kupitia Sheria ndogo za Halmashauri na kushauri endapo kuna mabadiliko yanahitajika yafanyike na kutoa ushauri ushauri wa hatua zipi zifuatwe ili kukamilisha suala hilo.
Lakini pia kitengo kinakazi ya kupitia mikataba yote ya Halmashauri na kutoa ushauri ,lengo likiwa ni kuokoa Hasara ambazo zinaweza kuipata Halmashauri.
Mwisho ni kutoa ushauri wa kisheria kwa menejimenti ya Mkurugenzi juu ya shughuli mbamabali za kiutawala na kiutendaji ili kutimiza malengo Halmashauri ili kutima malengo Halmashauri iliyojiwekea.
Kwa mwaka 2016/17 Halmashauri ya wilaya ya Kaliua ilikuwa na kesi 16 kwa mchanganuo ufuatao:-
S/N
|
MAHALA KESI ILIPOFUNGULIWA
|
NAMBA YA KESI
|
HATUA KESI ILIPOFIKIA
|
01
|
Mahakama Kuu kanda
ya Tabora
|
11/2015
|
Imeisha Na Halmashauri
imeshinda kesi hii na kuokoa mil 200.
|
02
|
Mahakama
Kuu kanda
ya Tabora
|
04/2017
|
Bado inaendelea..
|
03
|
Mahakama
ya Hakimu
Mkazi Tabora
|
43/2016
|
Imeisha
kwa
Halmashauri
kukubali kulipa
deni inalodaiwa.
|
04
|
Mahakama
ya Hakimu
Mkazi Tabora
|
Kesi
ya
Uchaguzi Na.03 ya
2015
|
Halmashuri
ilishinda kesi hiyo.
|
05
|
Mahakama
ya wilaya
Urambo
|
34/2015
|
Halmashauri
imeshinda kesi
na kuokoa mil
zaidi ya 400.
|
06
|
Mahakama
ya wilaya
Urambo
|
03/2017
|
Bado inaendelea..
|
07
|
Mahakama ya
wilaya Urambo
|
08/2016
|
Kesi
imeondolewa
kwanza Mahakamani.
|
08
|
Mahakama ya
wilaya Urambo
|
09/2016
|
Kesi
imeondolewa
kwanza Mahakamani.
|
09
|
Mahakama ya
wilaya Urambo
|
10/2016
|
Kesi
imeondolewa
kwanza Mahakamani.
|
10
|
Mahakama ya
wilaya Urambo
|
11/2016
|
Kesi
imeondolewa
kwanza Mahakamani.
|
11
|
Mahakama
ya wilaya
Urambo
|
12/2016
|
Kesi
imeondolewa
kwanza Mahakamani.
|
12
|
Baraza la Ardhi
na
Nyumba Tabora
|
129/2016
|
Kesi iliisha
kwa Halmashauri
kushinda kesi.
|
13
|
Baraza la Ardhi
na
Nyumba Tabora.
|
112/2017
|
Kesi bado inaendelea..
|
14
|
Baraza la Ardhi
na
Nyumba Tabora
|
130/2017
|
Kesi bado inaendelea..
|
15
|
Baraza la
Ardhi na
Nyumba Tabora
|
13/2016
|
Halmashauri
ilishinda kesi hiyo.
|
16
|
Baraza la
Ardhi na
Nyumba Tabora
|
37/2017
|
Halmashauri
imeshinda kesi.
|
Kuandaa sheria ndogo za Vijiji 100, kila kijiji Sheria 5, ambapo sheria hizo ni Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira, Sheria Ndogo ya Nguvu kazi, Sheria Ndogo ya Ushuru mbalimbali, Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kuzima Moto na Sheria Ndogo ya Maendeleo ya Elimu.
Pamoja na kuandaa Sheria Ndogo hizo Kitengo Cha Sheria pia kilipitia Sheria Ndogo za Halmashauri na kinaendelea na mchakato wa kuzihuisha kwani kuna mapungufu machache ikiwa nin pamoja na Kanuni za Kuendesha mikutano ya Halmashauri.
Zipo Rasimu za Sheria tatu ambazo ni Rasimu ya Sheria Ndogo za Kodi ya Majengo, Rasimu ya Sheria Ndogo ya Anuani ya Misimbo pamoja na Sheria Ndogo za Hifadhi ya Msitu wa Maboha -Mchakato bado unaendelea
Kupitia mikataba Mbalimbali na kutoa ushauri wa Kisheria kwa Halmashauri. Kwa mwaka 2016/2017 Kitengo cha Sheria kilipitia mikataba mikubwa ya Ujenzi minne (4), mikataba ya Benki Minne (4), mikataba ya simu miwili na mikataba midogo mchanganyiko zaidi ya sabini (70) ili kushauri nini kifanyike.
Kitengo cha Sheria pia kimetoa Msaada wa Kisheria kwa watu Mbalimbali ambao hawana uwezo wa kugharamia tozo za Mawakili ambapo kwa asilimia 90 Wahanga hao waliweza kupata haki zao mahakamani.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua