• Malalamiko |
    • MAWASILIANO |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Wafanyakazi |
Kaliua District Council
Kaliua District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu, na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Usafi wa Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Legal Unity
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji

Elimu Sekondari

IDARA  YA  ELIMU SEKONDARI

  • HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA ELIMU SEKONDARI KWA JAMII
  • Idara inashughulikia uhamisho wa wanafunzi ndani na nje ya wilaya.
  • Taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa ili mwanafunzi akubaliwe kuhama;
  • Barua ya Uhamisho
  • Iwe na anwani ya Mkuu wa Shule mwanafunzi anakohama na anakohamia.
  • Jina sahihi la mwanafunzi liandikwe (Majina matatu).
  • Iwe na namba ya kuandikishwa shuleni.
  • Ioneshe kidato anachosoma.
  • Iwe na mwezi na mwaka anaostahili kuhama.
  • Barua ya uhamisho ioneshe kuwa uhamisho utakamilika endapo TSM 9 itaambatanishwa au ikitumwa.
  • Kuwe na saini, jina na cheo cha aliyepitisha uhamisho (NB: Mkuu wa Shule halisi).
  • Kuwe na jina la mzazi au mlezi.
  • Barua inakilishwe kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ambako mwanafunzi anahama.
  • Fomu ya Uhamisho
  • Iwe na jina kamili la mwanafunzi (majina matatu).
  • Ioneshe kidato anachosoma.
  • Ioneshe mwaka wa kidato anachosoma.
  • Iwe na jina kamili la mzazi.
  • Ioneshe namba ya kuandikishwa shuleni.
  • Iwe na anwani ya mzazi au mlezi.
  • Kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu  ioneshe shule ya Msingi aliyosoma.
  • Kwa mwanafunzi wa kidato cha tano, fomu ioneshe shule ya sekondari aliyosoma kidato cha kwanza hadi cha nne.
  • Ioneshe mwaka aliopokelewa kidato cha kwanza au cha tano.
  • Ioneshe mchepuo.
  • Iwe na tarehe, jina, saini na mhuri wa mkuu wa shule anakohama na anakohamia mwanafunzi.
  • NB: Kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu, matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yaambatanishwe.
  • Ratiba ya Uhamisho
  • Uhamisho kwa kutumia fomu kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza ni kuanzia mwezi Juni kila mwaka. Kabla ya mwezi Juni uhamisho unafanywa na Afisa Elimu Mkoa.
  • Uhamisho unafanywa wakati wa likizo ya wanafunzi mwezi Desemba na Juni.
  • Uhamisho haufanywi mwezi Aprili hadi Mei na Oktoba hadi Novemba ili kuwezesha mwanafunzi kufanya mitihani katika shule anayosoma kabla ya kuhama.
  • Hakuna uhamisho wa mwanafunzi wa Kidato cha Nne na cha Sita.

 

  • Idara inapitisha maombi ya mzazi/mlezi anayeomba mwanae akariri darasa kutokana na sababu mbalimbali kama vile; ugonjwa, maendeleo duni darasani, na kadhalika.

Taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa ili mwanafunzi akubaliwe kukariri darasa ni;

  • Barua iandikwe na mzazi au mlezi
  • Barua ipitishwe na Mkuu wa Shule, Afisa Elimu Sekondari Wilaya  ndipo iende kwa Afisa Elimu Mkoa.
  • Ombi la kukariri darasa liwe na uthibitisho wa sababu za kukariri kama vile;
  • Ugonjwa - Kuwe na uthibitisho wa mahudhurio ya hospitali na mahudhurio ya shuleni. Mahudhurio hayo yawiane.
  • Maendeleo hafifu ya taaluma - Kuwe na uthibitisho wa taarifa ya matokeo ya kitaaluma pamoja na mahudhurio ya shule.

 

  • TAKWIMU ZA IDARA
  • Taasisi za Elimu
  • Kuna jumla ya shule za sekondari 14 ambazo zote ni za serikali na za mchanganyiko wa wanafunzi wa kike na wa kiume. Hakuna shule za binafsi. Shule hizo ni;
  • Igagala
  • Kaliua
  • Kanindo
  • Kapuya
  • Kashishi
  • Kazaroho
  • Mkindo
  • Mwongozo
  • Ugunga
  • Ukumbisiganga
  • Ulyankulu
  • Ushokola
  • Usinge
  • Uyowa

Kati ya hizo, shule 2 tu zinatoa elimu ya kidato cha Tano na cha Sita pamoja na elimu ya kidato cha Kwanza hadi cha Nne. Shule hizo ni Kaliua na Kashishi.

Sambamba na shule hizo 14 kuna kituo 1 cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (T.E.W.W) kinachotoa elimu ya sekondari kinaitwa Ulyankulu Open School, ni cha binafsi kinamilikiwa na kanisa Katoliki.

  • Idadi ya Wanafunzi
  • Ifuatayo ni idadi ya wanafunzi wa kidato cha Kwanza hadi cha Sita kama ilivyokuwa mwezi Machi 31, 2017
    • Kidato cha I-IV
    • Kidato cha V-VI
    • Jumla Kuu
    • Wav
    • Was
    • Jml
    • Wav
    • Was
    • Jml
    • Wav
    • Was
    • Jml
    • 3867
    • 2660
    • 6527
    • 343
    • 206
    • 549
    • 4210
    • 2866
    • 7076

    • Idadi ya Walimu
    • Jedwali lifuatalo linachanganua idadi ya walimu kama ilivyokuwa mwezi Machi 31, 2017
      • Shahada
      • Stashahada
      • Jumla Kuu ya Walimu
      • Sayansi
      • Sanaa
      • Sayansi
      • Sanaa
      • Sayansi
      • Sanaa
      • Wote
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • Me
      • Ke
      • Jml
      • 17
      •  
      • 2
      • 19
      •  
      • 134
      • 56
      • 190
      • 29
      • 5
      • 34
      • 88
      • 44
      • 132
      • 46
      • 7
      • 53
      • 222
      • 100
      • 322
      • 268
      • 107
      • 375

      • TAARIFA ZA MIRADI
      • Idara inaendesha miradi ya ujenzi wa shule mpya 8 za sekondari katika kata zifuatazo;
      • Ilege
      • Sasu
      • Kamsekwa
      • Isike
      • Kanoge
      • Zugimlole
      • Igwisi
      • Silambo
      • Idara inasimamia umaliziaji wa maabara ya shule ya sekondari Mkindo na uwekaji wa samani na matanki ya maji safi na taka katika maabara 42.
      • Idara inasimamia ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za sekondari Kaliua na Igagala.
      • Idara ina simamia umaliziaji wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya sekondari Kapuya.
      • TAARIFA ZA UTEKELEZAJI MAJUKUMU YA IDARA
      • Kusimamia utekelezaji wa mtaala (ufundishaji na ujifunzaji).
      • Kuratibu na kuendesha mitihani na upimaji.
      • Kukusanya, kuhakiki, kuchambua, kutunza na kutoa takwimu.
      • Kusimamia utawala bora katika shule.
      • Kuratibu michezo.
      • Kusimamia ubora wa mazingira ya kutolea elimu.
      • Kusimamia wajibu na haki za walimu, watumishi wasio walimu na wanafunzi.
      • MASWALI YA WANANCHI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KWENYE IDARA
      • Wananchi walio wengi wanaofika katika Idara ya Elimu Sekondari wanauliza maswali ya;
      • Taratibu za uhamisho.
      • Taratibu za kukariri darasa.  

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KALIUA DC MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II November 17, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA May 25, 2022
  • Ona zote

Habari za Hivipunde

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA DEREVA WA MTAMBO DARAJA LA II {GREDA} NAFASI 01

    May 04, 2025
  • MNADA WA KWANZA WA ZAO LA KARANGA WILAYA YA KALIUA

    March 24, 2025
  • MADIWANI KALIUA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA BAJETI YA BILION 50.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    January 30, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUPITIA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII IMETOA HUNDI YA TSH. 302,000,000/=

    December 23, 2024
  • Ona zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Kaliua 2018
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mwanzo
  • TAMISEMI
  • Huduma
  • Historia
  • Fursa za Uwekezaji
  • UTUMISHI

Kurasa zinazofanana

  • Salary Slips Portal
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya RC Tabora
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti za Serikali
  • Baraza la Mitihani - NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

MAWASILIANO

    Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni

    Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua

    Simu: +255262965676/9

    Dawati la Uwekezaji:

    Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz

Dawati la Malamiko

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Service

Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua