Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Bw. Shabani A. Kabelwa amewataka wanufaika wa Mikopo ya asilimia kumi (10%) inayotolewa na Halmashauri, kutumia kidogo na kuwekeza kikubwa ili kuweza kufikia Malengo yao na kurejesha marejesho kwa wakati
Ameyasema hayo leo tarehe 06/02/2026 katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua alipokua akizungumza na Vijana wa Kikundi cha Bodaboda cha Igagala City kilichopo Kijiji cha Mtakuja Maghalibi, kata ya Igagala, ambao wamekopeshwa na Halmashauri Pikipiki zenye thamani ya Tsh. 35,000,000/=
‘Tusidharau kazi maana kazi ni kazi cha msingi kila mmoja wenu azingatie maadili, na tujitambue kwenye namna nzuri ya kufanya matumizi ya fedha zetu, na ili ufanikiwe lazima kile unachokitumia kiwe kidogo kuliko kile unachokitumia, amesema Bw. Kabelwa
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi, Mjumbe wa kikundi hicho cha Igagala City Ndugu Thomas J. Sanda amesema wao kama vijana wapo tayari kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilikujikwamua kimaisha na kuweza kufaya marejesho kwa wakati.
Ikumbukwe kuwa huu ni mwendelezo wa utoaji wa mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa Mapato yake ya ndani na kwa kipindi cha Mwaka 2025/2026 imekwisha kutoa kiasi cha Tsh. 718,900,000.00
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua