Waziri wa Nchi TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo ameiponngeza Halamshauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa vitendo. katika ziara yake wilayani Kaliua tarehe 6/6/2020,, Mheshiwa Jafo ametoa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali wilayani kaliua yenye thamni ya Shilingi milioni 215. Pia Mheshimiwa Jafo amegawa pikipiki 10 kwa vijana wa bodaboda stand mpya Kaliua zenye thamani ya shilingi milioni 25 na vifaa vya vikundi ya viwanda vidogovidogo vyenye thamani ya milion 92. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 584. Aidha, Mheshimiwa Jafo ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wialaya ya Kaliua na kuzitaka halmashauri zingine kuiga mfano wa Kaliua
.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua