Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru umefika wilayani Kaliua tarehe 13/7/2021 na kuzindua pamoja na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ikiwemo; Uzinduzi wa mradi wa Pikipiki 30 katika Kata za Sasu, Usenye na Nhwande, Uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Kituo cha Afya Uyowa, Uzinduzi wa mradi wa maji ya bomba katika Kijiji cha Kasungu, Kutembelea mradi wa CCTV Camera Stendi ya Mabasi Kaliua, na Uzinduzi wa mradi wa Mnara wa TTCL Kaliua. Hata hivyo miradi yote imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi. Pamoja na hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru aliipongeza Wilaya ya Kaliua kwa kuzingatia kwa vitendo Kauli mbiu ya Mwenge Maalum wa Uhuru kwa kufunga CCTV Camera stendi ya Mabasi.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua