Halmashauri ya wilaya ya Kaliua imeshika nafasi ya nane (8) kati ya halmashauri 185 nchini katika utoaji wa mikopo ya 4% wanawake, 4% vijana na 2% valemavu kutoka kwenye mapato yake ya ndani. Katika mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri imetoa jumla ya shilingi milioni 454 zilizokopeshwa kwa vikundi 106.
Tuzo hii imekabidhiwa leo tarehe 28 Novemba 2018 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mkutano uliowakutanisha wataalamu na wadau wa maendeleo ya jamii nchini unaoendelea jijini Arusha.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Afisa maendeleo ya jamii Bi. Mwanahamisi Ally amesema kuwa tuzo hii ni kutoka na ushirikiano wa watumishi wa Halmashauri chini ya Uongozi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
“Shukrani za pekee ziende kwa Dr. John Pima kwa kutuwezesha katika kutimiza majukumu, shukrani kwa CMT yote, Kamati ya Mikopo, Maafisa maendeleo ya Jamii. Hakika ni jambo la kujivunia mshikamano wetu.” Alimalizia
Katika tuzo hizo pia mkoa wa Tabora umeshika nafasi ya pili huku Mkoa wa Songea ukiongoza kwa kutoa mikopo vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua