*Mwanafunzi Zugimlole-Kaliua aingia kumi bora.
*Wilaya ya Kaliua ya kwanza kimkoa, ufaulu 82.12%.
Akizungumza baada ya Baraza la Mitihani kutangaza matokeo, Kaimu Mkuu wa Idara Elimu-Msingi Bw. Robert Sanduli ameeleza kuwa mafanikio haya yametokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali ikiwa ni Wanafunzi, Wazazi , Walimu, Maafisa Elimu Kata, watumishi wote wa idara za elimu msingi na sekondari pamoja na serikali vijiji na kamati za elimu za vijiji katika kusimamia masuala ya elimu hasa katika kupambana na utoro na mimba za utotoni.
“Kwa kiasi kikubwa tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri Dr. John Pima pamoja na Mkuu wa Wilaya Abel Yeji Busalama kwa kuweka mikakati, miongozo na usimamizi wao madhubuti katika sekta ya elimu” Alisema Sanduli.
Katika mafanikio ya matokeo mradi wa EQUIP ambao umetoa mchango mkubwa kwa kuwa wezesha Maafisa Elimu Kata (waratibu)kuweza kuzifikia shule zote na kusimamia malengo ya Halmashauri.
Kaimu Afisa Elimu Sanduli ametoa wito kwa wadau wote ili kuendelea kupandisha ufaulu na kuwasisitiza wazazi kuwa wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2019 waanze kuwafanyia maandalizi mapema.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua