Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Dkt. khamis Mkanachi ambae amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.Paul Matiko Chacha kwenye Uzinduzi wa utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi kwa makundi Maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya kaliua katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vizuri Mapato ya ndani na kutoa asilimia kumi kwa Makundi maalumu kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya chama cha Mapinduzi.
‘’Jumla ya fedha iliyotengwa ya kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni mia mbili kwaajili ya mikopo hii ya asilimia kumi kwa awamu hii ya kwanza Milioni mia tatu na mbili ni sehemu ya Fedha inayokwenda kuwanufaisha wanufaika wa mikopo hiyo ambao ni Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu’’
Dkt. Khamis ameendelea kusema fedha hizi za mikopo zimekuja zikawasaidie watanzania kwani huu ndio mpango na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenda kuwasaidia Wananchi na kubadili maisha yao.
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Jafael Lufungija amewaomba Wananchi kuendelea kuwa wazalendo katika ulipaji wa Tozo ambazo Halmashauri imeidhinisha katika maeneo ya Wilaya yetu
‘’Tukiona mtu anakwepa kulipa tozo tumuone ni sababu itakayo tupelekea tuikose ile asilimia kumi kutoka Mapato ya ndani kwa maana ya asilimia nne kwa Vijana, asilimia nne kwa Wanawake pamoja na asilimia mbili kwa Watu wenye mahitaji maalumu’’
Kwa awamu hii ya kwanza Jumla ya Vikundi 10 vimepokea hundi hiyo ikiwa ni Vikundi 7 kwa Wanawake na Vikundi 3 kwa Vijana.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua