Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua inatekeleza agizo la Serikali na kuanza zoezi la upandaji miti katika taasisi za serikali. Zaidi ya miti 5,000 inatarajiwa kupandwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dr. John Marco Pima akishirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya wameongoza watumishi kwenye zoezi la upandaji miti lililoanza leo jumanne tarehe 12 Desemba katika zahanati ya Kaliua. Aidha Dr. Pima ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika zoezi hilo na kuitunza miti ili yote iweze kukua na kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutunza mazingira.
Kwa upande wake Katibu Tawala Ndugu Simon Nyehunge amewashukuru watumishi kuitikia agizo na kushiriki katika zoezi hili kwa kujituma.
"KALIUA TUNATEKELEZA"
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua