Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya bilioni 50.2 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Awali akisoma mapendekezo ya rasimu hiyo kwenye kikao cha baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Afisa Mipango Fransiska Mhagama amesema bilioni 7.6 ya bajeti hiyo ni fedha ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha akizungumza mara baada ya baraza la Madiwani kujadili na kupitisha rasimu hiyo ya bajeti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mh. Jafael Lufungija amesema asilimia 60 ya fedha kwenye bajeti hiyo zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, ambapo upande wa sekta ya afya zimetengwa million 80.
Pamoja na bajeti hii kugusa kila sekta, baadhi ya Madiwani wameeleza vipaumbele vinavyopaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee kwenye maeneo yao ambapo Diwani wa kata ya Zugimlole Mh. Barikeka Ramadhani amegusia kipaumbele cha ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo, huku Diwani wa kata ya Kaliua Mh. Nestory Hoka akizungumzia changamoto ya Upungufu wa Madawati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mh. Dkt. Gerald Mongella ameendelea kusisitiza usimamizi wa Miradi ya Maendeleo huku akisikitishwa na baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua