Wilaya ya kaliua ina jumla ya shule za msingi 100 zenye vyumba vya madarasaa 625.Idadi hii inafanya uwiano wa chumba kwa wanafunzi kuwa 1:104 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa wa 1:45. Jumla ya vyumba vinavyohitajika ni 1,730 hivyo kufanya kuwa na upungufu wa vyumba 1,105.
Madawati ya wanafunzi yaliyopo ni 12,543 na hivyo kufanya uwiano wa dawati kwa wanafunzi kuwa 1:5 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa ambao ni 1:3. Idadi ya walimu waliopo ni 1,826.kati yao wanawake ni 661 na wanaume ni 1,165.Idadi hii inafanya uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kuwa 1:39.Aidha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni 1:4
Kwa upande wa nyumba za walimu, kuna nyumba 320 wakati mahitaji ni nyumba 1,820. Aidha matundu ya vyoo kwa wanafunzi yapo 835 ukilinganisha namahitaji ya matundu 3,231.
Kwa wastani udahili wa wanafunzi kiwilaya upo katika kiwango cha 67.2% wakati kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la VII ni 41% na darasa la IV ni 87%
Kwa upande wa elimu ya watu wazima, kuna wanafunzi 412 waliojiunga na madarasa ya MEMKWA. Aidha Wilaya ina chuo 1 cha ufundi stadi (VETA) ambacho kiko eneo la Ulyankulu.
Kiwango cha watu wanaojua kusoma na kuandika katika umri wa miaka 5 na kuendelea ni 77%. Jitihada zaidi zinahitajika ili kuboresha huduma za elimu katika Wilaya ya kaliua.
Wilaya ya kaliua ina jumla ya shule za sekondari 14 zenye vyumba vya madarasa 110. Idadi hii ya vyumba vya madarasa inafanya uwiano wa darasa kwa wanafunzi kuwa 1:57 ukilinganisha na uwiano wa kitaifa ambao ni 1:40 hivyo kufanya wilaya kuwa na upungufu wa madarasa 50.
Kati ya Kata 28 za kielimu zilizopo,ni kata 13 tu ndizo zenye shule za sekondari wakati sera ya elimu ni kila kata kuwa na shule ya sekondari.Ujenzi wa shule za sekondari katika Kata 7 unaendelea.Kata ambazo ujenzi unaendele ni pamoja na Kamsekwa, Silambo, zugimulole, Igwisi, Kanoge, Seleli na Sasu Kwa upande wa nyumba za walimu,kuna jumla ya nyumba 63 wakati mahitaji halisi ni 413. Maabara zilizopo kwa sasa ni 42 ambapo kwa shule zilizopo zinatosheleza mahitaji.
Idadi ya walimu wa sekondari waliopo ni 413 na kati yao walimu 278 ni wanaume na 135 ni wanawake. Idadi hii ya walimu inafanya uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kuwa 1:16. Uwiano wa kitabu kwa wanafunzi ni 1:2 kwa vitabu vya masomo ya sayansi na 1:3 kwa masomo ya sanaa. Idadi ya viti vya wanafunzi vilivyopo ni 6,287 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 153.
Kwa upande wa mabweni, Wilaya ina jumla ya mabweni 17 kati ya mahitaji ya mabweni 99. Aidha kiwango cha wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito ni 0.04%.Kwa wastani ufaulu wa mitihani ya taifa kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni 69.62%,kidato cha sita ni 96% wakati ufaulu kwa kidato cha pili uko katika kiwango cha 79%. Jitihada zaidi zinahitajika ili kuboresha ubora wa elimu ya sekondari katika Wilaya ya Kaliua.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua