Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Watu wenye mahitaji maalumu Mh. Dkt. Dorothy Gwajima amefanaya uzinduzi wa shule ya Mpya ya Sekondari Usimba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Uzinduzi huo umefanyika tarehe 22/10/2024.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Gwajima amesema ujenzi wa shule ya Usimba ulikua ni mpango wa Wananchi wa Kata ya Usimba kwa kushirikiana na Halmashauri.
“Kama tulivyosikia kutoka kwa msoma taarifa, Wanachi hawa walikua na muhali wa kujenga Shule hii na hivyo wakapata uwezeshaji mkubwa kutoka kwa Serikali ya awamu ya sita hadi tunaiona Shule hii katika hatua hii fedha kiasi cha shilingi 653,890,562/= zimetumika ‘’
Aidha Dkt. Gwajima amesema Serikali ipo kwenye mpango wa kuleta Shilingi 500,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni, Nyumba za Walimu Pamoja na Madarasa mengine
‘’hivyo ndugu zangu nimekuja hapa kama Waziri wa maendeleo ya Jamii nimefurahi kile ambacho wanachi wamekiazinsha kimefanya Serikali yao iwaunge mkono nimeona Madaraa, nimeona Maabara nimeona miundombinu Mizuri na hivyo naamini baada ya miaka miwili hapa patakua tofauti sana”
Akizungumza kwa niaba ya Wanachi wa Wilaya ya Kaliua Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt.Gelard Mongella amesema uwepo wa shule hiyo katika Kata hii ya Usimba umerahisisha Watoto wa Maeneo hayo kupata huduma ya elimu kwa karibu kwani klabla walikua wanatembe umbali mrefu hadi kata Jirani ya Kazaroho Kwenda kusoma.
Ikumbukwe shule ya sekondari ya Usimba ilianza kujengwa mwaka 2022 kwa nguvu za Wananchi kwa kutoa eneo la ujenzi lenye ukubwa wa hekari 33 lenye thamani ya shilingi 300, 300,000/=.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua