Mkuu wa wilaya ya kaliua Mh. ABEL BUSALAMA leo amepoke mifuko ya simenti 200 kutoka katika kampuni ya ununuzi wa Tumbaku “ALLIANCE ONE – Tanzania Ltd” kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kaliua. Mifuko hiyo imekabidhiwa na mwakilishi wa Kampuni hiyo Bw. Deogratius Liso ikiwa ni moja ya misaada ambayo Kampuni hiyo imeahidi kusaidia katika wilaya ya Kaliua.
Akikabidhi mifuko hiyo mwakilishi wa “ALLIANCE ONE – Tanzania Ltd” Bw. Deogratius Liso alitoa shukrani kwa niaba ya kampuni kwa ushirikiano uliopo baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Kampuni hiyo katika uzalishaji bora wa zao la Tumbaku kwa wakulima wa eneo hilo. Pia mkuu wa wilaya ya kaliua Mh. ABEL BUSALAMA aliishukuru kampuni hiyo na kusema kwamba serikali imepokea msaada huo kwa dhati kabisa na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu na kampuni hiyo .
Pia katika makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya aliambatana na viongozi Mbali mbali wakiwemo Viongozi mbalimbali ngazi ya vijiji hadi wilaya wa Chama Cha Mapinduzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua (Dkt John M. Pima) na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kaliua (Mh. Haruna Kasele). Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 11.07.2017 siku ya jumatano saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Kaliua eneo ambalo linaendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo Wodi ya kinamama na jengo la OPD.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua