.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Ndugu Aggrey Mwanri amekabidhi vikundi vya wajasiriamali wilayani Kaliua hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 202. Fedha hizo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo 4% watapatiwa wanawake, 4% vijana na 2% walemavu.
Aidha Mkuu wa Mkoa kampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Ndugu John Marco Pima kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila mwezi wanatenga asilimia 10 ya mapato na kuiweka kwenye akaunti maalum.
Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa amemtaka mkurugenzi mtendaji kuzingatia vigezo vya mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na wakopaji kuwa katika vikundi, wakopaji kujulikana makazi yao na shughuli zao za uzalishaji wanazozifanya. Mwanri amevitaka vikundi kurejesha mikopo yao kwa wakati na kwa utaratibu utakaowekwa ili waweze kukopesheka zaidi, vilevile amewataka wajasiriamali kutumia vyema mikopo yao badala ya kuzifanyia hanasa badala ya malengo yaliyokusudiwa na watumie faida itakayopatika kuimarisha hali za familia kiuchumi.
Aidha mkuu wa mkoa amezindua jukwaa la wanawake ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Raisi ambalo litasaidia kuinua hali za kiuchumi kwa wanawake wilayani Kaliua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua alitangaza majina ya viongozi wa muda wa jukwaa kuwa; Mwenyekiti (Zainab Salum Andrea), Makamu Mwenyekiti (Teddy Mlekwa), Katibu (Anastazia Bebete), Katibu Msaidi (Mwajuma Mkwiti), Muweka Hazina (Bertha Samwel), Mjumbe (Joyce Springi). Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ameeleza kuwa jukwaa la wanawake litasaidia kutoa elimu, kurasimisha biashara ndogondogo, kukuza viwango vya bidhaa na kutoa mitaji na fursa za mitaji kwa wanawake.
Katika hafla hiyo Mh. Mwanri amekabidhi pikipiki nane kwa maafisa watendaji na maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Pikipiki nne zimekabidhiwa kwa maafisa watendaji na zingine zimekabidhiwa kwa maafisa ugani ili ziweze kuongeza tija kwa utendaji kazi wa watumishi hao na kusitiza kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Leo tunakabidhi pikipiki hizi kwa watumishi wachache lakini tutaendelea kuboresha kwa wengine kila tutakapopata fursa ya kufanya hivyo” Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua