Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Ndugu. Shabani Kabelwa tarehe 14/08/2025 amezungumza na Wakuu wa Shule zote za Halmashauri katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
Mkurugenzi Kabelwa amewahasa Walimu kuendelea kuishi Misingi ya Kazi na kufuata taratibu zote za kitumishi kwani kufanya hivyo kutarahisisha utoaji wa Huduma kwa Wanafunzi kama inavyotakiwa.
"Nendeni mkasimamie vizuri katika shule zenu, hakikisheni mnapandisha ufaulu kwa Wanafunzi lakini kumbukeni kuwakumbusha na kuwaelekeza Wanafunzi kuishi Mila na desturi za kitanzani" Amesema Mkurugenzi Kabelwa
Sambamba na hilo Ndugu. Kabelwa amewakumbusha Walimu kuendelea kuwa mfano Bora katika Jamii kwani Mwalimu ni kioo cha jamii.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua