Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Ndugu. Wenceslaus Melchior Lindi, Tarehe 26/09/2024 ametoa Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wananchi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.
Maelekezo hayo ameyatoa kwenye Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mh. Gerald Mongella, Wananchi pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa,.
Akitoa maelekezo hayo Ndugu. Lindi amesema;
“kwa mujibu wa kanuni ya 9 kanuni ndogo ya kwanza na ya pili A mpaka K ya kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa kitongoji za Mwaka 2024, Msimamizi wa Uchaguzi amepewa mamlaka ya kutoa Maelekezo kuhusu Uchaguzi na Maelekezo haya yanatolewa siku 62 kabla ya siku ya Uchaguzi”.
Akiendelea kusema Msimamizi wa Uchaguzi anasema maelekezo haya yanafafanua hatua zitakazo ongoza mchakato wa Uchaguzi kuanzia uandikishaji wa wapiga Kura, uchukuaji na urudishaji wa Fomu za Wagombea, uteuzi wa Wagombea na tarehe ya siku ya Uchaguzi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mh. Gerald Mongella ambaye ndiye alikua mgeni Rasmi amewapongeza Vyama Rafiki waliohudhuria zoezi hilo na kuwahasa kuwa kama Wilaya tunatakiwa kushikamana na kushiriki zoezi la Uchaguzi kwa Huru na Haki.
“Sisi kama Kaliua tunayo matarajio yetu katika kikao hiki cha maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ni kwanza kwa kuanza kama tulivyoanza hivi kwa ushirikiano na tuendelee na ushirikishwaji mpaka mwisho wa zoezi hili la Uchaguzi, kingine tunaomba kwa wakati wote Amani itamalaki”.
Ikumbukwe Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Jumatano ya Tarehe 27/09/2024 kwa Nchi nzima, huku Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakichagua Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua