Thursday 21st, November 2024
@BOMANI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua Dr. John Pima anapenda kuwatangazia wananchi wote maadhimisho ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kaliua.
Wananchi wote mnakaribishwa ili kuja kusikia na kujionea mafanikio kede kede yaliyofanyika kwa kipindi hiki cha miaka mitano. Sherehe hii itafanyika siku ya Jumapili tarehe 18 Novemba 2018 kwenye viwanja vya Makao makuu ya Halmashauri (BOMANI) eneo la Ufukutwa barabara ya Ulindwanoni. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.Aggrey Mwanri.
Wageni kutoka maeneo mbalimbali watakuwepo ya mkoa wa Tabora watakuwepo karibu tujumuike tusherehekee maadhimisho kwa pamoja.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua