Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilaya ya Kaliua na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mheshimiwa Abel Yeji Busalama leo tarehe 30/08/2019. Katika Wilaya ya Kaliua, Mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya msingi katika miradi yote ambayo ni; Zahanati ya kata ya Mwongozo, Bweni la Waschana Shule ya Sekondari Kazaroho, Mradi mkubwa wa Maji Kaliua Mjini, Ujenzi wa Ukumbi wa kisasa wa mikutano katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Kukagua zoezi la utoaji wa mikopo ya Pikipiki katika Kitongoji cha Mnange Kata ya Uyowa na, Kutembelea Jengo la Upasuaji Kituo cha Afya Kaliua pamoja na kutembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali ameisifia miradi yote na kukiri kuona thamani ya pesa katika iradi hiyo.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara ya Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255262965676/9
Dawati la Uwekezaji:
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua