Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ni Dr John Marco Pima. Kitaaluma, ni Mtafiti katika fani ya Sayansi ya Teknolojia ya Habari katika Nyanja za “Blended Learning”, Elimu Mtandao; “E-Government”; na “E-Records and Archival Management”. Dr. Pima anao uzoefu wa uongozi katika nafasi za uandamizi kwa zaidi ya miaka mitano na amepata mafunzo mbalimbali ya kiuongozi, kimkakati na kijamii. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kaliua, Dr. John Pima alikuwa Mhadhiri katika Chuo Cha Uhasibu Arusha tangu mwaka 2006. Dr John Pima anayo Shahada ya Uzamili (Masters) ya Sayansi ya Kompyuta toka Chuo Kikuu cha Coventry, Uingereza. Dr. Pima amehitimu Shahada ya Uzamivu (PhD in Computing) akibobea katika fani ya “Blended Learning” na “Collaborative Web Technologies”. Dr Pima amewahi pia kuwa Meneja wa TEHAMA (ICT Manager) katika Chuo Cha Uhasibu Arusha tangu mwaka 2012 hadi 2016. Amefanya tafiti mbalimbali na kuchaptisha maandiko yake katika majarida na makongamano ya kitaifa na kimataifa. Kwa sasa Dr Pima amejikita zaidi katika kusimamia maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
Ofisi zipo Eneo la Ufukutwa, Barabara Ulindwanoni
Sanduku La Posta: S. L. P 83 Kaliua
Simu: +255 622 225 618
Dawati la Uwekezaji: +255 627 052 034
Barua Pepe: ded@kaliuadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua